🔴#TBC: MUSUKUMA ATAKA WATEULE WANAOGOMBEA UBUNGE WAKAGULIWE NA CAG | KUTOKA #BUNGENI, DODOMA
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ ameishauri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia kwa Waziri wake, Mohammed Mchengerwa, kuwapima wateule wa Rais wanaotaka kugombea ubunge kabla ya kuruhusiwa.
Musukuma amerejelea kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Machi 11, 2025 akiwataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na watumishi wengine wa Serikali wanaotaka kujitosa katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu kutoa taarifa mapema, la sivyo watakosa vyote.