Ajira hewa Ughaibuni
Wakenya zaidi wamejitokeza kuelezea walivyohadaiwa na kuwachwa njia panda kwenye mpango wa serikali wa kuwatafutia ajira ughaibuni. Miezi sita baadaye, waliosimulia masaibu wanadai kulipa maajenti walioidhinishwa na serikali pesa kwa maandalizi ya kazi za ng’ambo ambazo hadi leo hawajaziona.