Aliyekuwa Rais wa Marekani Joe Biden apatikana kuugua saratani ya tezi dume
Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, amepatikana kuugua saratani ya tezi dume.
Kwa mujibu wa ofisi yake, Biden anaugua saratani ambayo imesambaa hadi kwenye mifupa yake.
Biden, ambaye aliondoka madarakani Januari anasema kuwa yeye na familia yake wangali wanatathimini aina ya matibabu atakayofanyiwa. Rais Donald Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii kwamba yeye mkewe Melania Trump wanasikitika kuhusu kuugua kwa Biden, na kumtakia ahueni ya haraka. Makamu wa Rais wa zamani Kamala Harris, ambaye alihudumu chini ya Biden, amesema kwamba yeye na mumewe Doug Emhoff wanaiweka familia ya Biden katika maombi yao.