Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Eldoret Kimengich ataka hospitali zinazohusishwa na uuzaji figo kufungwa
Sakata ya uuzaji wa figo imevutia hisia kutoka kwa makanisa huku kiongozi wa kanisa katoliki dayosisi ya Eldoret Dominic Kimengich akilaani wanaowahadaa wananchi kutoa figo. Askofu kimengich akizungumza mjini eldoret amesema hospitali zinazofanya upasuaji huo kwa kutozingatia kanuni na kwa kuhadaa wananchi zinastahili kufungwa mara moja. Kimengich pia amelaumu serikali kwa kuzembea na kuacha hospitali na watu binafsi kuendeleza biashara hiyo kwa kuhadaa wakenya na kuhatarisha maisha yao.