Baadhi ya viongozi wa Magharibi ya nchi waendelea kupinga ukodeshaji wa viwanda
Baadhi ya viongozi wa Magharibi ya Nchi wamemrai Rais William Ruto kusitisha mkataba wa kukodisha viwanda vya sukari kwa mwekezaji wa kibinafsi, Jaswant Rai . kulingana nao, uamuzi wa kukodisha viwanda hivyo ni dhihirisho kwamba serikali ya Kenya Kwanza imefeli kuzingatia manifesto yake hasa kipengele cha kufufua uchumi wa eneo la magharibi.