Baba Wadogo Kibra: Vijana wadogo kibra wamewachiwa mzigo wa kulea
Kwa miaka mingi, juhudi zimefanywa kupunguza mimba za utotoni miongoni mwa wasichana wadogo. Hata hivyo, sio mengi yamefanywa kuhusiana na watoto wa kiume, ambao sasa wamebainika kuwa na majukumu mazito ya kuwalea watoto wakiwa wachanga. Kwenye makala yetu maalum hii leo, mwanahabri wetu Brenda Wanga amefuatilia vijana wadogo waliolazimika kuwalea watoto wao peke yao, na anaangazia changamoto na mafanikio yao katika safari ya kuwa baba.