Faith Omollo alihukumiwa kifo nchini Malaysia baada ya kupatikana na hatia ya kuwa na dawa za Kulevy
Aliponea kunyongwa nchini Malaysia baada ya kupatikana na mihadarati alipowasili nchini humo kwa ahadi ya kazi. Hatia hii ikimuacha mkenya Faith Omollo kwenye gereza la Malaysia kwa miaka minane kabla ya rufaa yake kusikilizwa na kuwachiliwa kurejea nchini. Kwa Faith, masaibu yake yalianza na ahadi ya mapato mazuri ughaibuni huku akifichua kuwa aliwaacha wakenya wengine gerezani.