Familia za waliouwawa na magaidi Mandera zaomba msaada
Jamaa na marafiki wa watu watano waliuwawa baada ya kushambuliwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab katika kijiji cha Bur Abor kaunti ya Mandera sasa wanaomba msaada wa kifedha wa kusaidia familia za waliopoteza wapendwa wao.
Jamii hizo ambazo zingali kwenye hali ya mshtuko wanaomba serikali zote mbili kuwasaidia kwani watu hao watano walikuwa na familia changa na walikuwa wakitegemewa kwa kiasi kikubwa. Aidha, wanaomba serikali kuimarisha hali ya usalama katika machimbo ya mawe ambayo yako mbali na maafisa wa usalama ili kuokoa maisha ya wale wanaofanya kazi huko.