Gachagua amemlaumu Ruto kwa kuendesha serikali visivyo
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amesisitiza kuwa muungano wao na viongozi wengine wa upinzani utahakikisha kuwa rais william ruto ameondolewa mamlakani katika uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza kaunti ya nyandarua ambapo alihudhuria ibada ya jumapili na baadaye kuhutubia umma eneo la maili nne, gachagua ameongeza kuwa serikali ya kenya kwanza imekuwa ikiwahadaa wakenya kuwa watafadhili miradi ambayo haipo.