Gavana Fernandes Barasa aahidi kuzindua ligi kuu ya tamasha ya mapigano ya mafahali
Gavana wa kakamega fernandes barasa aliongoza awamu ya pili ya tamasha ya mapigano ya fahali huko Solyo eneobunge la Shinyalu.
Gavana Barasa aliahidi kuzindua ligi kuu ya pigano la fahali litakalojumuisha mafahali wote kutoka kaunti zote 12 za kaunti ya kakamega . Kulingana naye, hatua hiyo inatarajiwa kuhifadhi utamaduni wa jamii ya waluhya na kukuza utalii.