Kenya yapoteza shilingi bilioni 6 kwa kulipa faini
Mkaguzi wa pesa za serikali Nancy Gathungu sasa amefichua kuwa wakenya wamepoteza takriban shilingi bilioni sita kutokana na malipo ya faini ya pesa za ufadhili wa miradi ambazo hazikutumika kwa muda unaofaa. Akizungumza mbele ya kamati ya bajeti, gathungu amesema kuwa kuna utepetevu mkubwa serikalini ambapo wizara tofauti wanatumia mbinu mbalimbali kufuja pesa za umma.