Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka adai njama ya kumkamata Gavana Natembeya
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ameonya tume ya kukabili ufisadi nchini – EACC- dhidi ya kutumiwa vibaya na serikali kuwakandamiza magavana. Akizungumza baada ya hafla ya kutawazwa kwa Canon Patrick Kyalo Munuve kama askofu mpya wa kanisa la ACK huko Machakos, Kalonzo amesema kuwa viongozi wa upinzani watamtetea Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, ambaye wanadai amepokea ilani ya kupekuliwa kwa nyumba yake na makachero wa EACC. Kalonzo alizungumza saa chache kabla ya maafisa wa EACC kuvamia nyumba ya Gavana Natembeya.