Mafuriko yasababisha hasara kaunti ya Mombasa
Mvua inayoendelea kunyesha kaunti ya Mombasa imesababisha mafuriko katika mitaa mingi kaunti hiyo. Eneo bunge la Nyali ndilo lililoathirika zaidi huku baadhi ya wanafunzi wakikosa masomo kutokana na mafuriko. Aidha barabara za Links, Beach road na Mto Ndia zimekuwa kero kwa madereva na magari.