Mahakama yawapa dhamana maafisa wa KWS wanaohusishwa na kupotea kwa mvuvi Brian Odhiambo huko Nakuru
Maafisa sita wa shirika la huduma za wanyamapori wanaodaiwa kumteka nyara mvuvi Brian Odhiambo wameachiliwa kwa dhamana. Hakimu mkuu wa mahakama ya Nakuru Kipkurui Kibellion amesema kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuendelea kuwazuilia sita hao.