Mama ateseka akiwalea wasichana wawili wenye Tawahudi
Familia nyingi kutoka maeneo ya vijijini zilizo na watoto wenye tatizo la kupooza ubongo ama tawahudi, zinaendelea kulalamika, huku zikiitaka serikali kuimarisha huduma za afya kwa watoto hao. Mwanahabari wetu Chrispine Otieno, alitembelea familia moja katika eneo la bonchari, kaunti ya kisii, ambayo inakumbana na changamoto za kulea watoto hao baada ya kumpoteza mlezi wao mkuu.