Mashirika ya Haki yanataka polisi kuwajibika zaidi kwa mauaji ya GEN-Z
Mashirika ya haki nchini sasa yanataka mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuweka bayana orodha ya watu walioshtakiwa kuhusiana na mauaji ya vijana wakati wa maandamano ya Gen Z mwaka jana. Shirika la Amnesty International likirejelea ripoti ya punde zaidi ya upekuzi wa shirika la habari la BBC ulioonyesha wazi maafisa waliohusishwa na mauaji ya vijana hao.