Mmea wa 'Ipomea' wasambaa kwa kasi kaunti ya Kajiado
Huku magugu aina ya IPOMEA yakizidi kutatiza shughuli za ufugaji katika kaunti ya Kajiado, Mashirika mbalimbali sasa yameanza mikakati ya kusaidia jamii kupambana na magugu hayo ambayo yamesambaa kwa zaidi ya asilimia 70 katika kaunti hiyo. Mikakati hiyo ni pamoja na kuwapa wanajamii kiinua mgongo ili kuwavutia kushirikiana katika kazi ya kung’oa magugu hayo.