Mtaji wa Biashara Kajiado
Wizara ya vyama vya ushirika inaongoza zoezi la usajili wa vijana, wanawake na walemavu kunufaika na mradi wa mtaji wa kuanzisha biashara. Mradi huu wa Nyota unaofanywa kwa ushirikiano na ofisi ya mbunge wa Kajiado Kusini inanuiwa kuimarisha nafasi za kujiajiri miongoni mwa makundi haya.