Mwanafunzi wa gredi ya pili afariki maji Nakuru
Mwanafunzi wa gredi ya pili katika shule ya msingi ya Lenana jijini Nakuru amefariki baada ya kusombwa maji alipokuwa anatoka shuleni jana jioni. Familia ya mwanafunzi huyo Glen Karanja ilikuwa inamsubiri nyumbani walipofahamishwa kuhusu tukio hilo.