Mzozo wa 'Rombo Group Ranch' waibuka tena
Mzozo kati ya usimamizi na wanachama wa Rombo Group Ranch, mpakani mwa kaunti za Kajiado na Taita Taveta, umeibuka tena licha ya agizo la mahakama la mwaka jana kusitisha shughuli zote kwenye ardhi hio yenye ekari 100,000.