Papa Leo XIV ashinikiza wanahabari wanaozuiliwa gerezani kuachiliwa
Papa Mtakatifu Leo wa Kumi na nne amewataka wanahabari zaidi ya 500 waliofungwa kwenye magereza mbalimbali ulimwenguni kuwachiliwa huru. akizungumza kweenye kikao na zaidi ya wanahabari 6,000 mjini vatican,Roma, Papa Leo ameyataka mataifa yanayowazuilia wanahabari kuheshimu uhuru wao na kuwaacha watekeleze kazi zao za kuangazia matukio katika jamii.