Serikali inalenga kupunguza muda wa kozi za ufundi
Serikali inalenga kuimarisha Sekta ya masomo ya ufundi nchini ili kuwa na wafanyakazi bora .
Haya ni kwa mujibu wa katibu katika wizara ya elimu kwenye Idara ya Elimu ya Ufundi Esther Thaara Muoria,baada ya mkutano na Walimu wakuu wa vyuo vya ufundi kutoka eneo la magharibi uliofanyika katika chuo cha Kisiwa eneo Bunge la Kabuchai. Muoria amesema kuwa serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaosomeoa kozi za ufundi wanapata ajira baada ya kufuzu.