Serikali ya kaunti ya Busia yahusisha umma kwenye maamuzi
Mashirika yasiyokuwa ya serikali kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Busia yameanzisha mikakati ya kutoa hamasisho kwa wakazi kuhusu mswada wa kushirikisha umma kwenye maamuzi ya miradi ya kaunti. mchakato huo umeanza miaka sita baada ya mswada huo kuwasilishwa katika bunge la kaunti. Mswada huo unalenga kujumuisha mchango wa wakazi kwenye miradi na sheria za kaunti.