#TBC: DIAMOND AWAJIBU WANAOSEMA KAISHIWA KWENYE UANDISHI "MIMI NINA TALENT"
Msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amewajibu wakosoaji wanaodai ameishiwa ubunifu katika uandishi wa muziki.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Diamond amesema:
“Mimi naweza kuandika muziki wowote na kucheza na biti. Mimi nina talent. Silaha yangu kubwa ni kuandika.”
Kumekuwepo na mijadala mitandaoni kuhusu mwelekeo wa ladha ya muziki wake, huku mashabiki na wadau wakitofautiana kuhusu kazi zake za hivi karibuni hasa zenye ladha ya Amapiano.