Usaili wa makamishna wa IEBC
Mahojiano ya wawaniaji wa makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC yanaendelea huku watu sita zaidi wakiratibiwa kuhojiwa leo. Tayari wawaniaji wawili wamejiondoa kwenye mahojiano hayo. Wanaohojiwa leo ni Mary Karen Chesang Kigen, Mary Njeri Mburu, Melisa Yeko Ng’ania, Mohamed Adbullahi Abdi, Mohamed Ahmed Dagane na Mohamed Mahat Sabul.