Utaratibu wa kumpata Papa mpya
Papa Francis atazikwa chini ya siku sita kuanzia leo katika kanisa la St. Mary Major Basilica, tofauti na desturi ya MaPapa wengi waliozikwa katika kanisa la St Peter’s Basilica. Papa Francis ataombolezwa kwa jumla ya siku 9 huku Makadinali 135 walio chini ya miaka 80 wakitarajiwa kupiga kura ya kumchagua Papa mpya siku 15 au 20 baada ya kifo hicho kutangazwa.