Vijana wa Busia wajifundisha lugha ya Kijerumani
Zaidi ya vijana 700 kutoka kaunti za Nyanza wanakaribia kukamilisha awamu ya kwanza ya masomo ya lugha ya kijerumani ili kuwawezesha kupata ajira katika mataifa ya Ughaibuni. Ni mpango ulioanzishwa na serikali ya kitaifa kupitia kwa wizara ya usalama wa ndani ili kutafuta suluhu kwa changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana nchini.