Vikao vya umma kuhusu NG-CDF vimeanza leo nchini
Vikao vya maoni kuhusu mustakabali wa hazina ya CDF nchini vimeendelea sehemu nyingi nchini huku wengi walioshiriki wakitaka fedha hizi kusalia kwenye maeneobunge. Wengi waliozungumza kwenye siku ya kwanza ya vikao hivi sehemu mbalimbali nchini wamepinga kuondolewa kwa hazina hii na badala yake wakitaka fedha hizo kuongezwa.