Viongozi wa dini wakosoa wawakilishi wadi wa Nyamira kwa ugomvi
Muungano wa wachungaji katika kaunti ya Nyamira kwa mara ya kwanza umejitokeza kukemea mgogoro unaoendelea katika bunge la kaunti ya Nyamira, uliowagawanya wawakilishi wadi kwa mirengo miwili inayoandaa vikao sambamba katika maeneo tofauti kinyume na sheria.