Viongozi wa wanafunzi watishia kufanya maandamano
Uongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi umetishia kuanza maandamano juma hili baada ya Waziri wa Elimu Julius Migos kuwahamisha wanachama wanne wa baraza la chuo hicho lenye wanachama saba, siku chache kabla ya baraza hilo kuwa na kikao cha kuamua ni nani atakayechukua nafasi ya Naibu Chansela mpya wa chuo hicho mwishoni mwa mwezi huu