Wabunge watala Polisi kumkamata Gachagua
Wabunge sasa wanamtaka aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua kukamatwa mara moja na kushtakiwa kwa uchochezi kutokana na matamshi yake kwamba uchaguzi mkuu ujao utakumbwa na mchafuko. Wakiongozwa na kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichung’wah na mwenzake wa wachache Junet Mohammed, wabunge hao wanasema semi za Gachagua zitaleta janga la kitaifa iwapo hazitadhibitiwa.