Wafanyabiashara wasema hawakupewa sukari waliyonunua kutoka kwa kampuni ya Sony Sugar
Kizaazaa kilizuka wakati wa hafla ya kuikabidhi kampuni ya sukari ya Busia usimamizi wa kampuni ya sukari ya SONY baada ya wafanyabiashara wa sukari kutaka kurejeshewa pesa zao walizolipa kampuni ya Sony miezi mitano iliyopita bila matumaini ya kupata sukari.