Wahudumu wa afya wote waandamana
Maandamano hayo yalianzia eneo la Green Park hapa jijini na kisha kuelekea katika makao makuu ya wizara ya afya kabla ya kuelekea katika jumba la Delta Plaza ambako kuna afisi za baraza la magavana na hatimaye wahudumu hao kuelekeza maandamano katika majengo ya bunge.