Wakulima wa pamba wapewa mbegu zilizoboreshwa Busia
Ni afueni kwa wakulima wa pamba zaidi ya elfu moja katika maeneo bunge manne ya kaunti ya Busia baada ya kupewa ufadhili wa tani 10 za mbegu ya pamba iliyoboreshwa . Serikali kwa ushirikiano na kampuni ya Thika cloth mills inasambaza mbegu za pamba katika maeneo mbalimbali nchini .