Wanaume wawili wazozania mwili wa miaka 11 Mombasa
Utata umeibuka baina ya wanaume wawili wanaozozania mwili wa mtoto wa miaka 11 aliyefariki kwa njia tatanishi jijini Mombasa. Mwanaume mmoja anadai kuwa alimlea mtoto huyo kwa zaidi ya miaka 7 na hivyo anashikilia kwamba ndiye anapaswa kumzika Marehemu. Hata hivyo familia ya mamake mtoto huyo imemtetea baba mlezi wa sasa ikisema ndiye ana mamlaka ya kumzika mtoto huyo.