Watangazaji wa redio za Royal Media waungana na wakristo katika ibada za Pasaka
Kampuni ya Royal Media kupitia Radio Citizen iliungana na waumini wa Kanisa la Word of Faith mjini Mbale, Kaunti ya Vihiga, kusherehekea sikukuu ya Pasaka kwa kuadhimisha kufufuka kwa Yesu Kristo. Watangazaji wa Muuga FM na Ramogi FM pia walishiriki ibada maalum katika miji ya Siaya na Meru.