Watu watano wapigwa risasi na kuuawa na maafisa wa usalama eneo la Ang'ata Barikoi
Watu watano wamepigwa risasi na kuuawa na maafisa wa usalama kwenye zogo lililozuka eneo la Ang’ata Barikoi kaunti ya Narok kufuatia mzozo wa shamba. Mzozo huu uliosababishwa na ardhi ya ekari elfu sita ulisababisha watu wengine kumi wakiwemo maafisa wa GSU kujeruhiwa. Na kama Chrispine Otieno anavyoarifu, hali imesalia tete kutwa nzima kufuatia mzozo huu