Waziri wa Jumuia ya Afrika mashariki azindua miradi ya maji ya Emsoo na Chebagon, Elgeyo Marakwet
Waziri wa jumuiya ya afrika mashariki Beatrice Askul Moe amezindua miradi ya maji ya Emsoo na Chebagon pamoja na mpango wa upandaji miti shuleni katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Miradi hii ni sehemu ya jumla ya miradi 12 ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Bonde la Kerio (KVDA), ikiwemo mabwawa, visima na mitandao ya maji, kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 364.
Miradi ya maji ya Emsoo na Chebagon pekee imegharimu Shilingi milioni 100 na itanufaisha watu zaidi ya 13,000, taasisi na mifugo.