Wizara ya Leba yasema imetafuta kazi 500,000 ughaibuni
Wizara ya leba inasema kuwa serikali imetafuta nafasi elfu mia tano za kazi ughaibuni. Mutua amewatahadharisha vijana dhidi ya habari za kupotosha kuhusu kazi hizo akisema kuwa mipango ya kuwawasilisha walikosajiliwa kufanya kazi inaendelea. Aidha mutua amesema kuwa mawakala walaghai ndio wanaoiharibia jina serikali.