Zaidi ya Wafanyakazi 80 wamepoteza Ajira Dadaab
Athari za hatua ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ya kupunguza ufadhili kwa mashirika ya kimataifa yanayotoa huduma kwa wakimbizi zimeanza kushuhudiwa katika kambi ya Dadaab. Zaidi ya wafanyakazi 80 wamepoteza ajira baada ya kupunguzwa kwa rasilimali, hali inayozua taharuki miongoni mwa jamii ya wakimbizi na wahisani wanaotoa misaada.Wafanyikazi hao sasa wanatoa wito kwa mashirika ya kimataifa kuwajibika na kuhakikisha kuwa wafanyakazi waliopoteza kazi wanarejeshwa kazini au kusaidiwa kuanza maisha upya.